...Chezea Diamond wewe!
Watu weweee: Kila mmoja
akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond
wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka
wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya
kufuru stejini.
...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa
wake.
...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake
wa Nataka Kulewa.
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma
Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na
mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar
Live.
Vannesa Mdee akipelekeshana puta na Dimpoz
stejini.
KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi
mkali.
Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
Diamond akiwachizisha mashabiki.
Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
...Wakizidi kukonga nyoyo za
mashabiki.
Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar
Live.
Platnumz na dansa wake
kama 'The Wacko Jacko'.
Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa
akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na
Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi
(wa tatu kushoto).
Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha'
akikamua stejini.
...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe
"Wemaaaaaaaaaaaaa!"
Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas
ndani ya Dar Live.
Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na
shabiki jukwaani.
Pozi la Platnumz.
---
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia
leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa
Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa
na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha
pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya
Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha