Wednesday, June 26, 2013

Mama awaandalia mafunzo wanawake wajasiriamali jijini Dar es Salaam, yafunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Kigoda

 

 

Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa, akitoa hotuba yake  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda  akifungua mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. Mafunzo hayo  yanaendeshwa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), chini ya Mama Anna Mkapa.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda  akifungua  mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. 
Mwanamke mjasiriamali, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la 'Lady JayDee' akitumbuiza wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. Mafunzo hayo  yanaendeshwa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), chini ya Mama Anna Mkapa.
Mwanamke mjasiriamali, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la 'Lady JayDee' akitumbuiza wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. Mafunzo hayo  yanaendeshwa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), chini ya Mama Anna Mkapa.
Mwanamke mjasiriamali, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la 'Lady JayDee' akitumbuiza wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. Mafunzo hayo  yanaendeshwa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), chini ya Mama Anna Mkapa.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda wakiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi mbalimbali  pamoja na wafanyakazi wa EOTF  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda wakiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi mbalimbali  pamoja, wafanyakazi wa EOTF  na wanawake wajasiriamali  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani jijini Dar es Salaam leo. (Picha  zote na Magreth Kinabo - Maelezo)

Warembo wa Redd's Miss Temeke 2013, sasa hadharani



 Mrembo Jamila Ramadhan, akiwa katika pozi.
 Mrembo Hyness Oscar, akiwa katika pozi.
 Mrembo Margreth Olotu, akiwa katika pozi.
 Mrembo Latifa Mohamed, akiwa katika pozi.
 Mrembo Mutesi George, akiwa katika pozi.
 Mrembo Mey Karume, akiwa katika pozi.
 Mrembo Stella Mgazija, akiwa katika pozi.
 Mrembo Margreth Gerrad, akiwa katika pozi.
 Mrembo Axsaritha Vedastus, akiwa katika pozi.
 Mrembo Naima Ramadhan, akiwa katika pozi.
 Mrembo Irine Rajab, akiwa katika pozi.
 Mrembo Eastear Msulwa, akiwa katika pozi.
 Mrembo Svtlona Nyameyo, akiwa katika pozi.
 Mrembo Darlin Mmari, akiwa katika pozi.

Mrembo Narietha Boniface, akiwa katika pozi.


Baadhi ya washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao juzi.
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao. Kutoka kushoto, waliosimama ni Magreth OlotuNarieth Boniface, Latifa Mohamed, Mutesi George, Naima Ramadhan, Axarith Vedastus, Mey Karume, Easter Msulwa, Margreth Gerrad, Svtlon Nyameyo na walikaa chini ni Hyness Oscar, Jamila Ramadhan, Irine Rajab, Stella Mgazija na Darlin Mmari.
Baadhi ya warembo hao, wakipozi kwa picha kwenye mazoezi yao
Washiriki wa kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke 2013, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yao. Kutoka kushoto, waliosimama ni Magreth Olotu, Narieth Boniface, Latifa Mohamed, Mutesi George, Naima Ramadhan, Axarith Vedastus, Mey Karume, Easter Msulwa, Margreth

4 Wanyongwa nchini Nigeria



Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba.
Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji.
Shirika la Amnesty International lilisema kuwa hatua hiyo ya kuwanyonga wafungwa ni jambo la kuhuzunisha sana kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Nigeria.
Zaidi ya wafungwa 1,000 nchini Nigeria wanaaminika kuhukumiwa kifo .
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Rais Goodluck Jonathan hivi karibuni aliwataka magavana wa majimbo kutia saini vibali vya hukumu ya kifo katika jitihada za serikali kupunguza visa vya uhalifu.
Bwana Idahagbon alisema kuwa wananume wanne walinyongwa katika gereza la Benin baada ya mahakama kuamuru wanyongwe siku ya Jumatatu.
Alisema kesi zote za rufaa, hazikuweza kufua dafu na hukumu zao tayari zikuwa zimetiwa saini -mbili na magavana wa Edo Governor Adams Oshiomhole, huku nyingine zikitiwa saini na magavana wa majimbo mengine.
Ikiwa itathibitishwa , hatua hii ya kunyongwa ni ishara ya kurejea kwa sheria kali ya hukumu ya kunyongwa nchini Nigeria.
Wahudumu wa magereza ndio waliotekeleza hukumu ya kunyongwa , kitengo cha serikali wala sio jimbo la Edo.
Kulikuwa na ripoti za kutatanisha kuhusu hali ya mfungwa wa tano.
Chino Obiagwu wa kitengo cha sheria na mradi wa kuwasaidia wafungwa hao alisema kuwa mwanaume huyo alinyongwa.
Hukumu ilicheleweshwa kwa muda kwa sababu za kiufundi lakini baadaye wakapashwa habari kwa njia ya barua pepe, alisema bwana Obiagwu.
Lakini bwana Idahagbon alisema mwanaume huyo hakunyongwa kwa sababu hukumu yake ilisema kuwa auawe kwa kupigwa risasi.
Hata hivyo shirika la Amnesty International limesema kuwa limepokea habari zinazoweza kuthibitisha kuwa wafungwa wanne walinyongwa mjini Benin

MO AWA MTANZANIA WA KWANZA KUTAMBULIKA NA JARIDA LA KIMATAIFA LA FORBES AFRIKA

942331_578714148840668_773339795_n
Na Mwandishi Wetu
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

Mzee Mandela bado yuko hali mahututi

 


Hali ya Mandela inasemekana kuwa mbaya
Rais mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.
Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

Tuesday, June 11, 2013

Msanii Kashi Afariki Dunia

 

Habari zilizotufikia ni kuwa muigizaji wa filamu Jaji Hamisi maarufu kama Kashi amefariki dunia leo hii katika hospitali ya Muhimbili. bado hatujajua chanzo cha kifo chake lakini tutawaletea updates. Kashi alikuwa muigizaji mwenye kipaji cha hali ya juu katika filamu, pia aliwika na kundi la Shirikisho msanii Afrika lililokuwa linaonyesha michezo yake ITV.  Rest in peace Kashi

Msanii Kashi

Msanii Kashi

HATIMAYE H. BABA NA FLORA MVUNGI WAFUNGA NDOA

  

BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi, wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu.

H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.
 
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
“Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.


Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Akizungumza na mwandishi  wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana wakaamua kufanya maulidi tu.
 Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.