BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi, wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu.
H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.
“Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.
Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Akizungumza na mwandishi wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana wakaamua kufanya maulidi tu.
Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.
No comments:
Post a Comment