Friday, August 30, 2013

Mbunge wa Monduli CCM na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa asherehekea kuzaliwa kwake

 

Mbunge wa Monduli na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa akiwa na wajukuu zake tayari kukata keki ya sherehe ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake tarehe 26 aliyoandaliwa na mkewe mama Regina Lowassa huko Hekima Garden mikocheni.
 Wajukuu wakiiimba babu kata kekiii tuleeeeeee
  Bibi alisaidia kukata keki hiyo...
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akilishwa kipande cha keki na mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli. 

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akimlisha keki mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli.   

  Kumbato la pongezi kutoika kwa mkewe.
  Freddy nae akilishwa keki na baba.
 Mzee Lowassa akilishwa keki na mtoto wake Freddy Lowassa.
 
Babu akiwalisha keki wajukuu Makamanda wakiisubiri kwa hamu....

No comments:

Post a Comment