Thursday, December 27, 2012

DIAMOND,DIMPOZ WAFANYA KUFURU USIKU WA XMS DAR LIVE

 


...Chezea Diamond wewe!
Watu weweee: Kila mmoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa.
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
Vannesa Mdee akipelekeshana puta na Dimpoz stejini.
KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.
Kikosi cha Diamond Platnumz kazini.
Dimpoz na Vannesa Mdee wakimwaga nyuki stejini.
Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
Diamond akiwachizisha mashabiki.
Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
...Wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki.
Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
Platnumz na dansa wake kama 'The Wacko Jacko'.
Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi (wa tatu kushoto).
Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini.
...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaaaaaaaa!"
Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live.
Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na shabiki jukwaani.
Pozi la Platnumz.
---
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha

Waasi wanakakaribia kuingia Bangui


Wanajeshi wa Serikali ya CAR
Wanajeshi wa Serikali ya CAR
Hali ya wasi wasi imetanda katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Bangui, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kufika mji huo.
Mjumbe mmoja wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa ameshuhudia raia wa mji huo wakiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na na tishio la shambulio.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umewahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo, nayo serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo.
Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeagiza usalama kuimarisha katika ubalozi wake mjini Bangui, baada ya kushambuliwa na waandamanaji.
Waandamanaji hao walirusha mare ya kuchoma bendera ya Ufaransa.
Raia hao wanataka serikali ya Ufaransa kusiadia kuzima uasi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Wanadai serikali ya Ufaransa imewatekeleza.
Ufaransa ina takriban wanajeshi mia mbili mjini Banguia na utawala wa nchi hiyo umetoa wito kwa Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa waasi ambao wameuteka maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo.
Lakini rais wa Ufaransa Francois Hollande amekataa wito huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ameliambia shirika la Habari la Reuters kuwa mzozo huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

UZINDUZI WA GAZETI LA BURE LA MATANGAZO WAFANA DAR

 



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (kushoto), akiwa na Yakobe Chiwambo (kulia) mhariri mkuu wa gazeti jipya la matangazo la Dar Metro pamoja na Meneja Matangazo, Lightness Sirikwa wakiwa wameshikilia nakala za gazeti hilo wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika jana kwenye Mgahawa wa City Sports & Lounge, Dar es Salaam, Gazeti hilo litakalokuwa linatoka kila Jumatatu litagawiwa bure kwa wasomaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa gazeti jipya la matangazo la Dar Metro kwenye Mgahawa wa City Sports & Lounge, Dar es Salaama. Gazeti hilo litakalokuwa linatoka kila Jumatatu litagawiwa bure kwa wasomaji. Kutoka kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti hilo, Milka Nducu, Mhariri Mkuu wa gazeti hilo, Yakobe Chiwambo, Meneja Matangazo, Lightness Sirikwa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Peter Ambilikile.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwafrika Limited, Charles Sengo akisoma gazeti hilo wakati wa hafla ya uzinduzi.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa NBC, William Kallaghe akichangangia mawazo jinsi ya kuboresha gazeti hilo.
Mfanyabiashara wa vifaa vya umeme wa mionzi ya jua, Yonah Mushi akichangia kuhusu jinsi ya kuboresha gazeti hilo .
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya JCTL wakipata mlo wakati wa hafla hiyo

Rais Zuma matatani kuhusu madai ya Mbwa

 

Rais Jacob Zuma
Rais JJacob Zuma akicheza dansi
Serikali ya Afrika Kusini, imeelezea matamshi yaliyotolewa na rais wa nchi hiyo, ambayo yamewakasirisha watu wanaopenda mbwa.
Rais Zuma, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema umiliki wa mbwa ni itikadi za wazungu na sio mila na desturi ya waafrika.
Lakini msemaji wa rais huyo amesema, rais Zuma, alikuwa akionya watu kutowashughulikia zaidi wanyama kuluko binadamu wenzao na hakupendekeza au uashiria mbwa kutupwa.
Amesema ujumbe huo ulikuwa na ni\ ya kuhimiza raia kuimarisha utamdani wa kiafrika na kuondoa imani na fikra za kikoloni.
Gazeti la Mercury nchini humo limeripoti kuwa rais Zuma, aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara katika mkoa wa KwaZulu Natal kuwa watu wanaotumia pesa kununu mbwa, kuwapeleka hospitalini na kutembea nao, ni watu wanaoiga na kufuata maadili ya wazungu.
Gazeti hilo liliendelea kunadi kuwa rais Zuma alisema kuwa vijana wa taifa hilo wanajaribu kuiga mfumo wa maisha wa makabila mengine yasiyo ya Kiafrika.
'' Hata ukipata nywele zako mafuta ya aina gani, huwezi kuwa mzungu'' Gazeti hilo lilimnukuu rais Zuma.
Matamshi yake yamewagadhabisha watu wengi nchini humo ambao wamechapisha hisia zao katika ukarasa mbali mbali za mitandao ya kijamii.
Wanaharakati wanaotetea maslahi ya wanyama wameshutumu kwa kutoa matamshi ambayo hayapaswi kutolewa na kiongozi wa nchi huku wengine wametuhumu na ubaguzi wa rangi.

Baraza jipya la mawaziri latajwa Japan

Shinzo Abe
Waziri mkuu mpya wa Japana Shinzo Abe
Waziri mkuu mpya wa Japan, Shinzo Abe, ametangaza baraza lake jipya la mawaziri, huku akianza majukumu ya kuimarisha uchumi wa taifa hilo.
Baraza hilo la Mawaziri lilitanagzwa muda mfupi baada ya bunge la nchi hiyo kumuidhinisha Bwana Abe kuwa Waziri Mkuu, kufuatia ushindi wa chama chake katika uchaguzi mkuu mapema mwezi huu.
Chama cha Liberal Democratic na mshirika wake wana zaidi ya wabunge theluthi mbili katika bunge la wawakilishi
Bwana Abe, ambaye alikuwa waziri mkuu mwaka wa 2006-07, amemteua aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiy Taro Aso, kuwa waziri wa fedha.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, baraza hilo la mawaziri linajumuisha washirika wa karibu wa Bwana Abe, huku akianza mikakati ya kunusuru uchumi wa taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa Biashara na Viwanda Akira Amari, ameteuliwa kuwa waziri anayehusika na masuala ya uchumi naye mwanasiasa mkongwe Toshimitsu Motegi ameteuliwa kuwa waziri wa biashara.

 

Inakisiwa kuwa waziri huyo atakabithiwa jukumu la kubuni sera mpya kuhusu nishati kufuatia mkasa wa nuklia wa Fukushima uliotokea mwaka uliopita.
Bwana Abe, anakisiwa kuwa mwanasiasa asiyeegemea upande mmoja lakini aliondolewa madarakani baada ya umaarufu wake kushuka na alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Yoshihiko Noda
Aliyekuwa Waziri mkuu wa Japan Yoshihiko Noda
Lakini anarejea tena madarakani wakati mgumu na anakuwa Waziri Mkuu wa saba wa Japan, katika kipindi cha miaka sita.
Abe ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa waziri kuu wa nchi hiyo na mwanawe aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, amehaidi kuchukua msimamo mkali kuhusu mzozo wa mpaka na nchi jirani ya Uchina.
Serikali ya Uchina, imetoa wito kwa serikali mpya ya Japanm kuchukua maamuzi yanayoweza kutekelezwa kushughulikia mzozo kuhusu umiliki wa visiwa vya Mashariki ya Bahari ya Uchina.
Bwana Abe pia ametoa wito wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kujumuishwa kwa vipengee kuhusiana na uzalendo.
Chama cha LDP kilishinda chama tawala cha Democratic Party-DPJ katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 16 mwezi huu.
Kiongozi wa chama hicho cha DPJ Yoshihiko Noda, alijiuzulu baada ya chama chake kushindwa.

Wafuasi wa Morsi watoa wito wa umoja

Maandamano nchini Misri
Raia wa Misri wakiandamana
Wafuasi wa rais wa Mirsi Mohammed Morsi, wametoa wito kwa raia wote wa Misri, kushirikiana baada ya katiba mpya yenye utata kuidhinishwa.
Kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood, Mohammed Badie, amesema raia wote wa Misiri, wazee kwa kina mama, Wakristo na Waislamu ni sharti waanza mikakati ya kuujenga upya taifa lao, kwa hiari.
Zaidi ya asilimia sitini ya watu waliopiga kura wakati wa kura ya maamuzi waliunga mkono katiba hiyo, licha ya kuwa ni asilimia thelathini ya wapiga kura wote walishiriki katika zoezi hilo.
Wakosoaji wanasema, katiba hiyo mpya inawapendelea Waislamu na inahujumu azma na nia ya mageuzi ya kisiasa nchini humo.
Rais Hosni Mubarak, aliondolewa madarakani Februari mwaka wa 2011, baada ya kuwa uongozini kwa takriban miaka thelathini.
Baada ya kutolewa kwa matokeo ya kura hiyo ya maoni hiyo jana, mamia ya wapinzani wa katiba hiyo walifunga daraja moja katika mji mkuu Cairo huku wakiteketeza magurudumu ya magari na kukatiza shughuli za usafiri katika barabara hiyo.
Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood
Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura ya maoni
Uchaguzi wa bunge nchini humo sasa utafanyika katika miezi miwili ijayo.
Mgawanyiko ulioibuka baada ya kura hiyo ya maoni, umesababisha msukosuko wa kiuchumi na kuna ripoti kuwa raia wengi sasa wakibadilisha fedha zao na kuwa na dola za Kimarekani.
Kuna ripoti kuwa kuna uhaba mkubwa wa sarafu ya dola katika maduka ya forodha.
Kabla ya matokeo hiyo kutangazwa serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwa watu wanaotoka au kuingia nchini humo wataruhusiwa kubeba dola lefu kumi pekee kila mmoja.
Siku ya Jumatatu, benki kuu nchini humo ilitoa taarifa kuwa, ina hazina ya kutosha ya sarafu za kigeni kukithi mahitaji ya wote

Mlipuko mkubwa umetokea mjini Lagos

Mlipuko mjini Lagos
Maafisa wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka Lagos
Moto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.
Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.
Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.
Bado baadhi yamajengo yanaendelea kuteketea.
Mwandishi wa BBC anasema maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.
Kwingineko, maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi kubwa ya wakristo.
Msemaji wa jeshi ameiambia BBC, kuwa washambuliaji hao waliwafyetua risasi waumini katika kanisa dogo wakati wa ibada ya Krismasi.
Mshambuliaji mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Ripoti zaidi zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini kundi lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.