Sunday, January 27, 2013

HAPPY BIRTHDAY YA IRENE UWOYA NCHINI CYPRUS MIMI KAMA MMILIKI WA BLOG HII NAKUTAKIA MAFANIKIO MAZURI KATIKA MAISHA YAKO NAMI NIPO NYUMA YAKO KIMAOMBI NA KWA KILA UKIFANYACHO KAZI

HAPPY BIRTHDAY YA IRENE UWOYA NCHINI CYPRUS

Msanii nguli wa kike nchini Irene Uwoya amefanya Birtday party nyumbani kwake nchini Cyprus ya kutimiza miaka 21, Uwoya ameniambia anashukuru kufikisha umri aliofikia na anamshukuru mungu kwa kumfikisha umri huo vilevile bila kuwasahau wazazi wake waliomlea,Mume wake Hamad Ndikumana na wasanii wenzake kwa ujumla vile vile anawatakia Heri ya Mwaka mpya wenye mafanikio wasanii wenzake na wadau wote wa filam za kibongo na wapenzi wake wote wanaopenda kazi zake.Mimi kama THE GREATEST nakupongeza kwa kufikisha Umri huo,HONGERA

Irene Uwoya akikata keki kusheherekea kutimiza miaka 21 nyumbani kwake Nchini Cyprus

Akiwa makini kabisa katika kukata keki

Akipelekewa shampagne ili aifungue kuweka baraka katika sherehe hiyoShampagne zilifunguliwa watu wakapiga kelele kumtakia mafanikio mema kwa kutimiza miaka 21

Baadhi ya watu walioalikwa katika sherehe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Irene Uwoya

Picha ya kumbukumbu na mwalikwa


Irene Uwoya na mgeni wake

Irene Uwoya akiwa na mtoto wake wa kufikia

Mambo ya maakuli jamani,Dj akipata msosi kabla ajaporomosha mamboWatu wakipata menu

Wageni waalikwa wakipata misosi ya nguvu ndani ya party hiyo

Mambo ya misosi yakiendelea.....

Menu ilikuwa si mchezo jamani,Dada alijiandaa vilivyo

Picha ya pamoja na waalikwa wote waliohudhuria sherehe hiyo wadau mtakuwa mnajiuliza mumewe yuko wapi?Mumewe alikuwa nje ya mji katika majukumu ya kikazi si unajua soccer tena leo huku kesho kule

Baada ya mambo yote uliwadia muda wa kusakata dansi kama kawaida yake mtoto huyu hakusita kufungua muziki alijitoma mbele na watu wengine wakajiunga naye

Nyumba binafsi ya Zuma haina neno

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Afrika Kusini haukugundua ushahidi wowote kuwa fedha za taifa zilitumiwa kujenga nyumba binafsi ya Rais Jacob Zuma - swala ambalo limezusha utata kwa miezi kadha.

Rais Jacob Zuma

Lakini Waziri wa Ujenzi, Thembalani Thulas Nxesi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba zaidi ya dola milioni-7 za serikali zilitumiwa kuimarisha ulinzi kwenye nyumba hiyo ilioko Nkandla.
Kati ya kazi hiyo ilikuwa kujenga pahala pa helikopta kutua, zahanati na nyumba za kuishi walinzi wa rais.
Uchunguzi huo uliamua kuwa Rais Zuma hakuwa na kauli katika mipango hiyo ya usalama.

CLAUDS MEDIA YAUKARIBISHA MWAKA KWA SHANGWE KUBWA


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.
Boss Joe akiwaomba wafanyakazi wote wazinyanyue glassi zao za vinywaji juu na kuzigonganisha kwa pamoja kuonesha upendo,mshikamano na ushirikiano.Baada ya hapo Wafanyakazi walipewa ruksa ya kula kunywa na kujimwaya mwaya.
Shampeni ikimiminwa baada ya kufunguliwa.
Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.
Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.
Dj Zero akiangusha ngoma live ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2 usiku huu.
Baadae wafanyakazi wa Clouds Media Group walianza kupata chakula cha pamoja kama uonavyo pichani.
Kulia ni Paul James a.k.a PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2
Dj Mayanga akiangusha ngoma za kufa mtu usiku huu ndani ya Escape 2
Pichani kulia ni Dj Venture,Gerald Hando pamoja na Mdau mwingine.
Kulia ni Dj Too Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2.
Dj PQ aliyekaa wakipiga stori na sebastian Maganga pamoja na PJ.
Mzee wa Kipindi Cha Jahazi,Eprahim Kibonde na mdau mwingine wakipata vitu laini laini safi kabisa.
Ilikuw ni full kujichana,kula kunywa na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya hafla usikuu huu ndani ya Escape 2.
Dada Regina Mwalekwa akiwa amepozi na Bonge Barabarani.
Cheersssss
Pichani kulia ni mdau mkubwa wa Clouds Media Group,Dauda wa Kota akifurahia jambo na Dada Regina Mwalekwa.
Sehemu ya kikosi kazi cha Clouds Tv wakishangilia jambo.

Thursday, January 10, 2013

Sakata na mapenzi ya jinsia moja yaandama chuo kikuu cha Victoria

Tangazo katika gazeti la Uganda linalohimiza mswada huo kufutiliwa mbali
Chuo kimoja kikuu nchini Uingereza, kimesitisha uhusiano wake na chuo kikuuu kimoja nchini Uganda , kupinga uamuzi wa wabunge wa nchi hiyo wa kuidhinisha mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja.
Chuo kikuu cha wa Buckingham kisema kimesikitishwa na mswada huo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, kikisema kuwa kinakandamizi juhudi za kuafikiwa kwa uhuru wa kujieleza na ushirikiano.
Chuo hicho sasa kimestangaza kuwa kimesitisha ushirikiano wake na chuo kikuu cha Victoria.
Hata hivyo chuo hicho cha Buckingham, kimesema wanafunzi wanaoendelea na masomo yao kwa sasa hawataadhiriwa na uamuzi huo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chuo hichi cha kibinfasi, uamuzi huo umeafikiwa baada ya mazungumzo na shirika la Edulink, lililo na makao yake mjini Dubai, ambalo ni mmiliki wa chuo hicho cha Victoria.
Taarifa hiyo imesema kuwa chuo hicho kimeshindwa kutekeleza na kutimiza sheria za Uganda na Uingereza inayozuia ubaguzi.

Chuo cha Victoria hakitafungwa

Chuo kikuu cha Buckingham
Wasimamizi wa chuo hicho sasa wanesena kuwa ushirikiano wao na chuo kikuuu cha Burkingham umesitishwa rasmi.
Kufuatia tangazo hilo, chuo kikuu cha Victoria kitasitisha kutoa shahada katika masomo ya usimamizi wa biashara, uhasibu, uandishi wa habari na masomo ya teknolojia ya komputa hatua ambayo itawaadhiri takriban wanafunzi mia mbili.
Kaimu naibu wa Chansella wa chuo cha Victoria, David Young, chuo hicho kitaendelea kutoa mafunzo ya masomo mengine ikiwa na pamoja na sayansi ya utabibu na afya ya jamii ambayo shahada zake hazitolewi na chuo cha Burkingham.
Chuo kikuu cha Victoria, kilifunguliwa mwaka wa 2011, na rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na Chansela wa chuo hicho ni aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Apolo Nsibambi.

Wednesday, January 9, 2013

HONGERA SHAMSHA FORDI KWA KUMFANYIKA KITU CHA KIHISTORIA MWANAO TERRY,HAKIKA MIMI DOROTHY NISHABIKI WAKO NAMBAR ONE

 


Shamsa Ford juzi kati alifanya party kubwa kwa ajili ya mwanae kama shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kiumbe alichompatia nakuwaalika wasanii wanzake wengi ili kumpa sapoti kama kawaida ya Bongo Movie Unit kupeana ushirikiano pale linapotokea jambo tucheki mambo yalivyokuwa...

Shamsa Ford akiwa na mwanaye Terry Dickson.

Irene Uwoya akiwasili.

Shamsa pamoja na rafiki yake kipenzi Zamaradi Mketema mtangazi wa kipindi cha Take One mwenye top nyekundu wakiwa na mdau.

Ulifika wakati wa kufungua Shampeni , The Greatest niliwakilisha vyema.

Mambo yakiendelea kupamba moto..

JB pia,,,

Kwa upande wakina Dada waliwakilishwa na Davina.

Taratibu zikiendelea..

Ulifika muda wa Keki, Shamsa akimlisha mchumba wake Dickson


Irene Uwoya akila keki..

Ulifika muda wa Maya kula keki..

Mama wa Bongo Movie Eliethy Chumila naye akuwa nyuma katika upande wa keki

Cath Rupia.....

Mariam Ismail..

Ule muda muafaka wa The Greates kula keki ulifika.

Nikipata picha ya pamoja.


Mkurugenzi wa 5 Effect Wiliam Mtitu kwenye picha ya pamoja na Shamsa na mchumba wake.
Inno mdau namba moja wa Rj Company bila kukosa..

Mambo ya ulabu palikuwa hapatoshi wadau.

Msosi time.

Muda wa kutoa zawadi...

Kama kawaida ya Erick Ford( JB) kumwaga pesa kama njungu ni kawaida yake.

Juma Chikoka naye akuwa nyuma katika kutoa mkono wa pongezi

Taratibu za kutoa zawadi zikiendelea...

Batuli(Neshi) akimwaga madolari.

Davina naye akimwaga mvua ya pesa kwa Shamsa

Vivian naye akifanya mambo yake.

Rado akitoa shoo ya hatari sana...


Dickson Mchumba wa Shamsa akiongea machache kuwashukuru Bongo Movie na wadau wote.

Single Mtambalike akimwaga cheche zake.

The Greateast nami nikiongea machache.

Dick aliweza kufanya suprise kubwa ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake...

Akiwa na furaha kubwa...

Shamsa akitoa neno lake la shukrani kwa wadau wote walioudhuria party ya mwanae na kuelezea furaha aliyonayo baada ya kuvishwa pete ya uchumba.