Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya AC Milan na Pro Patria za
nchini Italia, ilisitishwa na ya wachezaji kutoka nje ya uwanja kwa sababu ya
kutolewa maneno ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi.
Mchezaji wa AC Milan Kevin-Prince Boateng alibeba mpira dakika ya 25 ya
mchezo na kuupiga kuelekea walikokaa watazamaji.Kumekuwa na kauli zilizotolewa zikiwataka mashabiki wa wachezaji kuacha kutumia lugha ya ubaguzi.
Akiwa anatoka uwanjani, Boateng aliwapongeza watazamaji waliokabiliana na vitendo vya ubaguzi vilivyoonyeshwa na baadhi ya mashabiki.
Baadaye ikafahamika kuwa mechi hiyo isingeendelea na tovuti rasmi ya AC Milan imesema wachezaji wengine weusi wa timu hiyo akiwemo M'Baye Niang, Urby Emanuelson na Sulley Muntari - walikabiliwa na vitendo vya ubaguzi uwanjani.
Koocha wa AC Milan, Massimiliano Allegri amewambia waandishi wa habari: "Tumesikitishwa na kuhuzunishwa kwa kile kilichotokea.
Mkurugenzi wa uratibu wa AC Milan Umberto Gandini ameiambia BBC Sport: "inasikitisha sana lakini tulitakiwa kuonyesha ishara kali. Tumefurahishwa sana na uamuzi wa wachezaji wote wa Milan wa kutoka nje ya uwanja."
Wachezaji wenzao , akiwemo nahodha wa Manchester City Vincent Kompany, wamemuunga mkono Boateng na wachezaji wenzake kwa uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment