Wapelelezi wameomba msaada wa kumfuatilia mtu mmoja
anayeaminika kukaidi amri ya Taasisi ya Kuzuia Ugaidi na Upelelezi ya Uingereza,
TPims.
Polisi wanasema Ibrahim Magag, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni wa asili ya
Somalia, "hafikiriwi moja kwa moja kuwa ni tishio kwa usalama wa umma nchini
Uingereza"Waziri wa Mambo ya Ndani James Brokenshire amesema: "hatuamini kutoweka kwake kuna uhusiano na mipango ya ugaidi nchini Uingereza."
Amesema: "Taasisi ya Kuzuia Ugaidi na Upelelezi katika suala hili ilitaka kumzuia mtuhumiwa kuchangisha fedha na kusafiri nje."
TPims inazuia uhuru wa kutembea kwa watu wanaofikiriwa kuhatarisha usalama wa umma, lakini ambao hawawezi kufunguliwa mashitaka kwa sababu za usalama wa taifa.
Utambulisho wa watu walio chini ya uchunguzi wa Tpims mara nyingi unafanywa siri, lakini usiri huu umeondolewa kwa Bwana Magag kufuatia ombi la polisi.
Polisi waliarifiwa kutoweka kwake"baada ya kushindwa kutii masharti ya kubakia ndani usiku kucha katika Siku ya Boxing Day.
'piga 999'
Idara ya Polisi kitengo cha kupambana na ugaidi kimewataka wananchi kupiga simu namba 999, wanapomwona, lakini wasimkaribie.''Usalama wa taifa, ni jukumu kuu la serikali na polisi wanafanya kila wawezalo kumkamata mshukiwa huyu haraka iwezekanavyo'' Alisema James Brokenshire waziri wa mambo ya ndani.
Bwana Magag, anasemekana kuwa mtu mwenye urefu wa futi sita na nchi mbili, ana umbo wastani, ndevu, lakini polisi wanasema huenda anajaribu kubadili jinsi anavyoonekana.
Mara ya mwisho mshukiwa huyo alionekana katika eneo la Camden majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini za Uingereza siku ya Jumatano.
Alikuwa amevalia suruali ya Khaki na sharti Nyeusi na nguo nyingine inayofanana na nguo za kijeshi.
Mwezi Machi mwaka huu ilibainika kuwa raia tisa walipewa masharti na polisi ya kutotembea maarufu kama Tpims.
Mwezi Juni mwaka huu mtu mwingine alifunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria kama hiyo.
Wale wanaoamriwa kutimiza sheria hizo hulazimika kukaa ehemu moja na kupiga ripoti katika kituo cha polisi kila siku.
Vikwazo vingine ni pamoja, na kutokutana na watu fulani na kwenda mahali fulani au kusafiri katika nchi za ng'ambo.
Polisi sasa wametoa wito kwa mtu yeyote mwenye habari kumhusu Bwana Magag, ambaye mara ya mwisho alionekana katika eneo la Camden siku ya Jumatano kuwasiliana na idara ya kupambana na ugaidi kupitia nambari 0800 789 321 au kuwasiliana na kituo chochote cha polisi kwa kupiga namba 999.
No comments:
Post a Comment