Takriban watu 8 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano
mapya eneo la Tana River kusini mashariki mwa Kenya. Taarifa hizi ni kwa mujibu
wa shirika la msalaba mwekundu
Mamia waliuawa mwaka jana katika mapigano mengine ya kikabila katika eneo
hilo.Watu wengine watatu walijeruhiwa vibaya , kwa kukatwa katwa na mapanga. Inaarifiwa kuwa hali ni ya wasiwasi huku kukiwa na tetesi za kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Polisi mmoja alithibitisha kuwa watu wanane waliuawa , tisa kujeruhiwa na kuwa nyumba ziliteketezwa wakati wa mashambulizi hayo.
Duru za polisi zilisema kuwa wale waliouawa ni watu kutoka jamii hizo mbili. Na idadi yao imefikisha idadi ya waliouawa tangu kuanza kwa mashambulizi haya ya kuvizia kati ya jamii hizi hadi watu 140.
Ni Chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuuu kufanyika Kenya kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa mwaka 2007 uliokumbwa na utata na kusababisha ghasia.
Ghasia hizi mpya zimesababisha wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama na uwezo wa polisi kuthibiti hali katika maeneo tete.
Mwezi Disemba pekee watu 45 waliuawa katika shambulizi lengine.
Jamii hizo zimewahi kupigana na mzozo wao umekuwa ukisemekana kusababishwa na mgogoro wa maji na malisho ya wanyama.
Lakini kwa sababu ya hali ya mashambulizi yenyewe, ambapo watoto na wanawake wamekuwa wakiuawa na nyumba kuteketezwa , imewashangaza wengi huku baadhi wakiwatuhumu wanasiasa kwa kuyachochea.
No comments:
Post a Comment