Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Afrika Kusini haukugundua
ushahidi wowote kuwa fedha za taifa zilitumiwa kujenga nyumba binafsi ya Rais
Jacob Zuma - swala ambalo limezusha utata kwa miezi kadha.
Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Afrika Kusini haukugundua
ushahidi wowote kuwa fedha za taifa zilitumiwa kujenga nyumba binafsi ya Rais
Jacob Zuma - swala ambalo limezusha utata kwa miezi kadha.
Lakini Waziri wa Ujenzi, Thembalani Thulas Nxesi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba zaidi ya dola milioni-7 za serikali zilitumiwa kuimarisha ulinzi kwenye nyumba hiyo ilioko Nkandla.
Kati ya kazi hiyo ilikuwa kujenga pahala pa helikopta kutua, zahanati na nyumba za kuishi walinzi wa rais.
Uchunguzi huo uliamua kuwa Rais Zuma hakuwa na kauli katika mipango hiyo ya usalama.
No comments:
Post a Comment