Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda
Issa Ponda akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
es Salaam leo pamoja na washtakiwa wenzake 49, hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa
kutokana na mashahidi upande wa mashtaka kutofika mahakamani hapo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa na mshtakiwa mwenzake, Mukadam Abdal Swalehe (kushoto)
Baadhi ya wafuasi wa Sheikh Ponda wakiwa katika
viunga vya mahakama ya Kisutu
Katibu Mkuu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na mshtakiwa
mwenzake Mukadam
Abdal Swalehe wakitoka mahakamani chini ya ulinzi wa askari
magereza.
Ulinzi uliimarishwa katika eneo la Mahakama ya
Kisutu leo.
Katibu Mkuu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na
washtakiwa wenzake.
No comments:
Post a Comment